Monday, March 11, 2013

UJENZI WA STENDI YA MKOA NA STENDI YA VIDALADALA YASABABISHA MSONGAMANO




Wakati mkoa wa Dodoma ukiendelea kukua kwa kasi kufuatia kuboreshwa kwaMiundombinu na ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani pamoja na ujenzi wa stendi ya Daladala maarufu kama JAMATINI umekuwa ni chanzo cha msongamano wa magari,abiria,wafanya biashara na vibaka hali ambayo nikero kubwa kwa wakazi Mkoa wa Dodoma. Mwandishi wetu alipozungumza na SUMATRA wao walisema:Tuliweka utaratibu mzuri wa daladala zilizohamishwa kutoka Jamatini nakwenda eneo la Reilway ilikupisha ujenzi wa kituo hicho cha daladala na mabasi yaendayo mikoani wao walipelekwa NANENANE sasa kama hawa wa mabasi yaendayo mikoani wamerudi eneo walipo hamishwa watakuwa wamekaidi agizo la Serikali.
Tulipozungumza na madereva wa mabasi yaendayo mikoani kwanini wamerudi eneo waliloondolewa wao walijitetea kwa kusema: Wametupeleka NANENANE pasipo kutuandalia mazingira kule hakuna huduma za kijamii abiria wanaonabora wsafiri na mabasi ambayo booking office zao zipo mjini kwahiyo sisi tuliopo nanenane tunakosa abiria ndio maana tumeona bora tuje tukomae hapa angalau abiria si haba. Abiria kilio cha kikubwa ni wezi wa mifukoni ambao wanawakosesha amani. Pia wafanyabiashara hususani MAMA NTILIE wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira hatarishi. HII NDIO DODOMA LAZIMA TUKUBALI SHIDA ILI IWE NA MUONEKANO WA MAKAO MAKUU YA TANZANIA.  
 KWA HABARI NA MATUKIO TEMBELEA  
WWW.SHAZI USWAZINI.BLOGSPORT.COM
Na Mwanahabari wako ABDUL RASHID MUSSABURUDANI MAKINI

No comments:

Post a Comment