Waliwavunjia soko la RAILWAY wakaenda nje ya soko la MAJENGO baada ya kuwafukuza wakahamiSABASABA na usiku wa kuamkia leo wamewavunjia na kusababisha hasara
kubwa kwa wafanyabiashara hao. Wakizungumza
na SHAZI USWAZINI wafanyabiashara
hao walikuwa na haya ya kusema: Manispaa wanatunyanyasa sana na hii ni kwa sababu
walipo tuvunjia Railway wakatupeleka CHADURU
sehemu ambayo ni kando ya mji na kama unavyojua biashara zetu zinahitaji sehemu
yenye mkusanyiko wa watu. Tukaamua tukabanane soko kuu Majengo walipo tufukuza
tulienda kwa mkuu wa mkoa kulalamika ndipo Manispaa wenyewe wakatuleta hapa
sabasaba chaajabu usiku wa leo wametuvunjia bila taarifa. Pia licha ya
kuharibiwa kwa bidhaa zao wanadai bidhaa zilizo haribiwa ni chache bidhaa
nyingi zimeibwa. Mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Mkurugenzi wa Manispaa
lakini hakufanikiwa kumpata. HAYO NDIO
YALIOWASIBU WAFANYABIASHARA WA ENEO LA SABASABA(DODOMA MJINI).
Nikweli Serikali Ina Nia Njema Na Wanainchi Wake?
Ukizingatia Soko La Ajira Ni Gumu Katika Nchi Yetu.Wananchi Wanapojiajiri
Inakuwa Vita Kati Yao Na Serikali..... Je Nini Kifanyike??? Unaweza Kututumia Maoni Yako Kupitia Account yetu ya facebook/CREYZ BEEZ..
Na
Mwanahabari wetu Abdul Rashid, kutoka Shazi Uswazini.
No comments:
Post a Comment